Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  limewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kujitolea  kuripoti  katika makambi waliyopangiwa kati ya Mei 7 hadi 14, 2021.

Uamuzi  huo umetolewa leo Ijumaa Aprili 30, 2021 na mkuu wa JKT, Meja Jenerali Charles Mbuge ikielezwa kuwa wanaotakiwa kuripoti ni wale wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne.

Akizungumzia uamuzi huo, Kaimu mkuu wa utawala  wa JKT,  Kanali Hassan Mabena amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti katika kambi walizokuwa awali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Jeshi hilo kusitisha mafunzo hayo Februari, 2021 na kuwarejesha vijana hao nyumbani.

“Vijana wenye elimu ya kidato cha sita ngazi ya cheti, stashahada, shahada na wenye taaluma ya uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa,” amesema Kanali

Samia aahidi ongezeko la mishahara, agusia malipo mafao ya wastaafu
Bashiru, Polepole 'out' CCM, hawa hapa warithi wao