Aliyekua rais wa FC Barcelona Joan Laporta ameitaka bodi ya klabu hiyo kujiuzulu, kufuatia kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kipindi cha msimu wa 2016-17.

Laporta ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, amesema rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu na jopo lake la uongozi wameshindwa kuitunzia heshima FC Barcelona kwa kuiwezesha kufanya vizuri ndani na nje ya Hispania.

Amesema FC Barcelona sio klabu ya kupoteza muelekeo wa kushindwa kufanya vyema katika ligi ya Hispania na barani Ulaya, kutokana na kuwa na kila kitu, ili kusaidia hatua ya kufikiwa kwa malengo.

Akitolea mfano katika utawala wake, Laporta amesema FC Barcelona ilijiweza kwa kila hali, na ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Hispania mara nne kati ya mwaka 2003-2010 alipokua madarakani.

“Endapo bodi yote itakubali kujiuzulu, nitakua tayari kusimama katika uchaguzi mkuu ujao,” Laporta ameliambia gazeti la The Guardian.

“Tatizo lipo kwenye bodi ambayo ukomo wake ni mwaka 2021. Kama watakubali kuondoka. Sitokua na shaka na mpango wa kuingia kwenye harakati za kuwania kiti cha urais, lakini kama wataendelea kwa miaka minne iliyobaki, sifikirii kufanya hivyo.

Wakati wa utawala wa Joan Laporta ambaye aliiongoza FC Barcelona kuanzia 15 Juni 2003 – 30 Juni 2010, alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Hispania (La Liga) mara nne (2004–05, 2005-06, 2008-09 na 2009–10).

Ubingwa wa kombe la Mfalme (Copa del Rey) mara moja (2008–09).

Ubingwa wa Supercopa de España mara tatu (2005, 2006 na 2009).

Ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) mara mbili (2005–06, 2008–09).

Ubingwa wa UEFA Super Cup mara moja (2009).

Ubingwa wa klabu bingwa duniani (FIFA Club World Cup) (2009).

Ahaha kufanya upasuaji kurudisha ‘bikira’ aokoe ndoa yake
Familia ya Ndesamburo yakanusha kuwepo mgogoro kati yake na Chadema