Rais wa mabingwa wa soka nchini Hispania (FC Barcelona) Joan Laporta ameahidi kumrejesha Pep Guardiola klabuni hapo, endapo atapata nafasi ya kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Laporta amewahi kuiongoza FC Barcelona kuanzia mwaka 2003 hadi 2010, na alikua chachu ya kumpandisha Guardiola kutoka kwenye kikosi cha vijana cha klabu hiyo hadi kuwa meneja mkuu wa kikosi cha wakubwa mwaka 2008.

Kwa sasa Guardiola ana mkataba na mabingwa wa soka nchini England (Manchester City) hadi Juni 2021, lakini kibarua chake kipo shakani kutokana na klabu hiyo kuwa kwenye kifungo cha kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kipindi cha miaka miwili, baada ya kubainika walikwenda kinyume na kanuni ya Financial Fair Play.

“Nitahakikisha ninapambana kufanikisha harakati za kumrudisha nyumbani Guardiola, najua wengi wanahisi kama ninatania lakini jambo hili litakamilishwa kwa uwezo wangu endapo nitapata ridhaa ya kuchaguliwa na kuwa Rais wa FC Barcelona,” alisema Laporta alipohojiwa na TV3.

“Nina uhusiano mzuri sana na Guardiola, ninaweza kumshawishi ili akubali kurudi hapa, nina imani atakapokua hapa kila kitu kitarudi kama zamani hususan kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, ambapo tulifanya vizuri sana wakati wa utawala wake kama meneja.”

“Mara kwa mara nimekua nikizungumza naye pale ninapohitaji kufanya hivyo, tunazungumza mambo mengi ya kimaendeleo kuhusu klabu yetu, nina uhakika kama nitakua Rais mipango yote tunayoizungumza tutaihamishia kwenye utendaji na mambo yatakua vizuri kuanzia mwaka 2021.” Alisema Laporta

FC Barcelona ilishinda mataji 14 – yakiwemo mataji matatu ya ligi ya Hispania, mataji mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya – wakati wa utawala wa Guardiola, ambaye aliamua kuondoka klabuni hapo mwaka 2012 na kutimkia kwa mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich na baadae kutua England kwa matajiri wa mjini Manchester (Man City).

Ruhsa kufanya mazoezi ya pamoja Italia
India yarudisha usafiri wa treni kwa tahadhari