Rais mteule wa Marekani Joe Biden amepata sindano ya kwanza kati ya mbili za chanjo ya virusi vya corona huku akitazamwa mubashara kwenye runinga.

Biden amesema ameamua kuchoma chanjo hiyo moja kwa moja kupitia runinga nia na madhuni ni kuwahakikishia wamarekani kuwa chanjo hiyo ni salama.

Mke wa Rais mteule Jill Biden pia alipokea chanjo hiyo katika hospitali iliyo karibu na makazi yao, ambapo baadhi ya viongozi waliopata chanjo ni pamoja na Makamu wa Rais Mike Pence na Spika wa Bunge Nancy Pelosi.

Wakati huo huo Biden, aliwataka raia wa Marekani kuvaa barakao na kuepuka safari zisizo za lazima katika kipindi cha sikuku.

Hata hivyo Rais wa nchi hiyo Donald Trump, ambaye mwezi Oktoba alikutwa na Virusi vya Corona bado hajasema ni lini amepanga kupata chanjo hiyo.

Sambamba na hilo Shirika la Afya Duniani WHO limetahadharisha dhidi ya wasiwasi wa kupindukia kuhusu aina mpya ya virusi vya corona vinavyosambaa kwa kasi kubwa, baada ya kugunduliwa nchini Uingereza na baadae Afrika Kusini.

Vifo vitokanavyo na ajali vyapungua mwaka 2020
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 22, 2020