Beki wa klabu ya Liverpool Joe Gomez amelazimika kuondoka katika kikosi cha timu ya taifa ya England, kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uholanzi uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa kutoka ndani ya chama cha soka nchini humo (FA) zimeeleza kuwa, Gomez ameondoka kambini na kurejea kwenye klabu yake ya Liverpool kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Beki huyo mwenye umri wa miaka, 20 alifanyiwa mabadiliko katika dakika 10 za mwanzo za mchezo dhidi ya Uholanzi siku ya ijumaa, na tayari ameshafanyiwa vipimo baada ya kuwasili katika kituo cha mazoezi cha Liverpool (Melwood training ground).

“Joe Gomez amerejea Liverpool kwa ajili ya matibabu zaidi, baada ya kuumia kifundo cha mguu alipokua katika jukumu la kuitumikia timu ya taifa dhidi ya Uholanzi,” zimeeleza taarifa zilizochapishwa katika akaunti ya Twitter ya timu ya taifa ya Engand.

Timu ya taifa ya England ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki fainali za kombe la dunia za 2018, na itaanza kampeni za kuwania ubingwa wa dunia kwa kucheza dhidi ya Tunisia Juni 18, na baadae itapambana na Panama pamoja a Ubelgiji katika kundi G.

 

Obama na mkewe waunga mkono maandamano
Kocha Taifa Stars atamba kuibuka na ushindi dhidi ya DR Congo, kesho.