Klabu ya Burnley imethibitisha kumsajili aliyekua mlinda mlango chaguo la kwanza katika timu ya taifa ya England Joe Hart, akitokea kwa mabingwa Manchester City, kwa mkataba wa miaka miwili.

Usajili huo unafungua ukurasa mpya wa maisha ya soka kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye anaondoka Man City baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 12, huku akitwaa mataji mawili ya ligi kuu ya England na kombe la chama cha soka FA.

Kusawili kwa meneja Pep Guardiola kulivuruga mipango la mlinda mlango Hart kudumu kwa muda mrefu ndani ya Man City, kutokana na kutoridhsihwa na mwenendo wake wa kulinda lango la klabu hiyo, hali ambayo ilimfanya ampeleke kwa mkopo nchini Italia katika klabu ya Torino msimu wa 2016/17, na msimu wa 2017/18 alifanya hivyo akiwa na klabu ya West Ham Utd ya England.

“Kusajiliwa kwa Hart kunaendeleza hatua ya kukitanua kikosi chatu na kuwa na uwezo wa wachezaji ambao wataleta upinzani katika kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza, hali hii tunaamini itafanikisha lengo la kuwa na kikosi imara kwa msimu wote.”

Tunaamini uwezo wa mlinda mlango Nick Pope, lakini ujio wa Hart utaendelea kudhihirisha ubora wake kwa kuhakikisha anaendelea kuwa chaguo la kwanza katika kipindi hiki.” Imeeleza taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya klabu ya Burnley.

Wanachama CCM wamkataa mbunge kutoka Chadema
Jack Butland kuziba pengo la Thibaut Courtois