Mlinda mlango kutoka nchini England Charles Joseph John (Joe Hart), ameripotiwa kuwa kwenye harakati za kufanyiwa vipimo vya afya huko jijini London kwenye makao makuu ya klabu ya West Ham Utd.

Mlinda mlango huyo, anatajwa kuwa katika mpango huo, kufuatia kushindwa kumshawishi meneja wa klabu ya Man City Pep Guardiola baada ya kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Torino ya Italia.

Hart mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo jumatatu, na kama atafanikiwa kukidhi vigezo, atasajiliwa na wagonga nyundo wa jijini London West Ham Utd.

Taarifa za mlinda mlango huyo kuwa kwenye mpango wa kufanyiwa vipimo vya afya, zimetolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, mapama hii leo.

Nolito Arudi Nyumbani Hispania
Lowassa autaka tena urais mwaka 2020

Comments

comments