Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amelazimika kumuondoa kikosini mlinda mlango wa Man City, Joe Hart kufuatia majeraha ya mguuu alioyapata wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini humo dhidi ya Man Utd uliochezwa mwishoni juma lililopita.

Hodgson, amefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kwamba Hart, hatoweza kuwa sehemu ya kikosi chake ambacho kitaikabili Ujerumani mwishoni mwa juma hili, kabla ya kupambana na Uholanzi juma lijalo katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Kufuatia maamuzi hayo, kocha huyo mwenye umri wa miaka 68, amemuita mlinda mlango wa klabu ya Burnley, Tom Heaton kuziba pengo la Hart ambaye huwa chaguo lake la kwanza.

Tom Heaton is back in England's squad

Mlinda mlango wa klabu ya Burnley, Tom Heaton.

Katika hatua nyingine Hodson, amethibitisha kumuondoa mshambuliaji wa Man City, Raheem Sterling ambaye pia aliumia katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Man Utd.

“Haiwezi kuwa furaha kuwakosa Joe Hart na Raheem Sterling kwenye mchezo dhidi ya Ujerumani na Uholanzi, tumewaita wengine kama mbadala wao”

Kikosi cha timu ya taifa ya England kilichosalia, kuelekea katika michezo hiyo miwiwli ya kimataifa ya kirafiki, upande wa makipa yupo Jack Butland (Stoke City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley)

Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jagielka (Everton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)

Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool).

Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City), Theo Walcott (Arsenal), Danny Welbeck (Arsenal).

Abdi Banda Amvuruga Kocha Wa Simba Jackson Mayanja
Nahodha Wa Stars Aliwasili Kabla D’jamena – Chad