Kiungo wa klabu ya Crystal Palace Joe Ledley amefikia lengo la kucheza fainali za Euro 2016, kufuatia hatua ya kupona kwa wakati majeraha ya mguu aliyoyapata wakati wa michezo ya mwisho ya ligi ya nchini England.

Ledley alitajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales mnamo May 7, licha ya kukabiliwa na majeraha ya mguu, lakini kocha mkuu wa timu hiyo Chris Coleman, aliamini muda wa kupona kwa kiungo huyo bado ulikua unatosha.

Ledley, mwenye umri wa miaka 29, alifanyiwa vipimo na imeonekana amepona kwa wakati na anaamini atakuwa sehemu ya wachezaji watakaoipa mafanikio timu ya taifa ya Wales ambayo itakua ikishiriki kwa mara ya kwanza fainali za mataifa ya Ulaya.

Uwepo wa kiungo huyo kikosini kumemuongezea kujiamini kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales kuelekea katika fainali za Euro 2016, ambapo watapambana na Russia, Slovakia pamoja na majirani zao England katika michezo ya kundi B.

Wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Wales ni mshambuliaji wa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid Gareth Bale, David Cotterill (Birmingham) pamoja na George Williams (Fulham).

Slaven Bilic Ajitosa Kwa Carlos Bacca
Rais wa zamani wa Chad ahukumiwa ‘Kifungo cha maisha jela’

Comments

comments