Kiungo wa klabu ya Crystal Palace, Joe Ledley ameingia katika hali ya sintofahamu ya kuzikosa fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 (Euro 2016) zitakazofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao.

Ledley, ambaye ni raia wa nchini Wales, amefanyiwa vipimo na kubainika aliumia kisigino alipokua katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England wa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Crystal Palace walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Stoke City.

Taarifa zilizothibitishwa na kuchapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Crystal Palace, zimeeleza kwamba, kiungo huyo huenda akawa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu, hivyo ana hatihati ya kuzikosa fainali za Euro 2016.

Hata hivyo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman alimuacha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, kwenye kikosi chake cha awali ambacho kimesheheni wachezaji 23.

Mbali na kufikiriwa huenda akazikosa fainali za Euro 2016, Ledley ameingia mashakani kuukosa mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la FA, ambao utawakutanisha dhidi ya Man Utd, Mei 21 katika uwanja wa Wembley.

Arsene Wenger Amtengea Kiungo Wa Uswiz Mamilion Ya Pauni
Mark Clattenburg Akabidhiwa Dakika 90 Za Mchezo Wa Fainali