Timu ya Sevilla CF ya nchini Hispania usiku wa kuamkia hii leo ilinyakua ubingwa wa Europa League kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Liverpool mabao matatu kwa moja katika uwanja wa St. Jacob Park jijini Basel, Uswis.

Liverpool ambao waliunza mchezo kwa kasi kipindi cha kwanza ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 kupitia kwa Daniel Sturridge baada ya kupokea pasi kutoka kwa Phillipe Coutinho.

Kipindi cha pili kilipoanza mshambuliaji Kelvin Gameiro aliisawazishia Sevilla baada ya kupokea pasi toka kwa Mariano huku magoli mengine yakifungwa na Coke dakika ya 64 na 70.

Kolo Toure (right) consoles Liverpool team-mate Philippe Coutinho after defeatKolo Toure (kulia) akijaribu kumfariji mchezaji mwenzake wa Liverpool  Philippe Coutinho baada ya kupoteza mchezo wa hatua ya fainali usiku wa kuamkia hii leo.

Pamoja na kupata mabao hayo, pia mabingwa hao wa kihistoria walionekana kucheza vizuri kwa muda mwingi kipindi cha pili na kuwafanya majogoo wa Anfield kushindwa kuwazuia wanapofika langoni kwao.

Sevilla CF imenyakua taji hilo mara nne ndani ya miaka 10 tangu 2006. Imechukua ubingwa huo mwaka 2006, 2014, 2015 na 2016.

Stand Utd Wajipanga Na Msimu Wa 2016-17, Watano Watemwa
Young Africans Kurejea Dar es salaam Kesho