Wenyeji katika kijiji kimoja cha Luanda Kaunti ya Vihiga nchini Kenya waliachwa na mshangao mkubwa na kuchanganyikiwa baada ya jogoo anayedaiwa kuibwa katika Kaunti nyingine kukataa kuuzwa licha ya bei yake nafuu.

Mwizi aliyekuwa amemleta jogoo wa kuiba katika soko la Luanda alijikuta matatizoni baada ya kutaka kumuuza jogoo huyo na alichanganyikiwa kama walivyochanganyikiwa wengine, baada ya kugundua kuwa, Jogoo huyo kutoka Kaunti ya Siaya, alimkatalia mwizi (kwa jina William) kila mara alipotaka kumuuza.

Tukio hilo lilitokea na kujirudia mara 4 hadi watu waliokuwa sokoni walipoanza kushuku na kuamua kumkabili mtu huyo na kumhoji kumhusu jogoo huyo ambaye bei yake ilikuwa ndogo tofauti na ukubwa wa jogoo.

Wafanyabiashara katika soko hilo, walimhoji William na kutaka kufahamu ni kwa nini jogoo huyo alikuwa akionyesha tabia isiyokuwa ya kawaida na alishindwa kuwajibu kwa ufasaha.

Baada ya muda wakimhoji, kumbe taarifa ilikuwa imemfikia mwenye jogoo ambaye alifika na hatimaye kumtambua kuku wake aliyekuwa ametoweka kwa kuwa soko hilo lipo mpakani, inadaiwa mwenye kuku huyo alikuwa amefika katika soko hilo na alikuwa akimsaka kuku huyo.

Katika hali ya kushangaza sana, mtu huyo alisema amefanya urafiki mkubwa na mifugo wake, na kwamba ni vigumu mtu yeyote kumwibia na aliondoka na kuku wake huku mhusika wa wizi akiponea kichapo kwa kupigwa na umma.

Hata hivyo, ilidaiwa mwenye jogoo huyo ni mganga ambaye nguvu zake na dawa zilichangia kuku huyu kukataa kununuliwa kwani sio hali ya kawaida.

'Huddah The Boss' aangukia kwa Mwanariadha Omanyala
ASFC: Simba SC Vs Young Africans kupigwa CCM Kirumba