Joh Makini amezungumzia sababu zinazofanya video za muziki wa wasanii wa Hip-Hop nchini kukosa wafuatiliaji wengi kwenye mtandao wa Youtube, ukilinganisha na video za wasanii wanaoimba.

Joh makini ambaye video yake mpya ‘Kata Leta’ aliyomshirikisha Davido kutoka Nigeria imetizamwa mara756,411 ndani ya wiki tatu, amesema anadhani sababu kubwa ni kwamba mashabiki wengi wa muziki huo ni watu wa maisha ya kawaida, hivyo hawaingii sana mtandaoni.

Akizungumza na Amplifier ya clouds Fm, rapa huyo amesema hashangai kuona video zake na za wasanii wengine wa muziki wa Hip-Hop nchini hazifatiliwi na watu wengi kwenye Youtube kama ilivyo kwa wasanii wa muziki wa kuimba kwa sababu mashabiki wao ni watu wa mitaani.

“Sababu Mashabiki wengi wa Hip-Hop ni watu wa mtaani ambao sio watu wanaoingia sana mtaani, labda hiyo inaweza kuwa sababu ya video nyingi za Hip-Hop kukosa watazamaji wengi ‘’ amesema Joh.

Hata hivyo, zipo video chache za hip-hip ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na hata kuzifunika baadhi ya nyimbo za bongo fleva zilizotoka wakati huo.

Video ya Roma ambayo ina wiki moja tangu imetoka imetazamwa mara756,411. ‘Chuma Ulete’ ya Rayvany wa WCB imefuatiliwa mara 752,643 ikiwa na wiki mbili tangu imetoka, wakati.

Meya wa jiji la Dar awataka wananchi kutunza miundombinu
Wazee walalamikia malipo TASAF, wadai yasilipwe kwa mtandao