Mweusi Joh Makini amekamilisha video ya wimbo wake aliofanya na mshindi wa tuzo ya MTV/MAMA kutoka Afrika kusini, rapa AKA.
Video ya wimbo huo unaoitwa ‘Don’t’ Bother’ aliomshirikisha pia member wa kundi la Weusi, G Nako, imetayarishwa na muongozaji Justin Campos anaeheshimika zaidi Afrika kwa ubora wa video zake. Hii itakuwa collabo kubwa zaidi ya kimataifa aliyowahi kufanya Joh Makini.
Hivi karibuni, Joh Makini na G Nako walienda nchini Afrika Kusini kushuti video ya wimbo huo uliotayarishwa na Nahreel ndani ya studio za The Industry.