Mkongwe wa filamu za bongo, Johari Chagula amewataka wakazi wa Mbeya kukaa mkao wa kula katika tamasha la Nyumbani Festival litakalofanyika siku ya Idi Mosi kwenye ukumbi wa Royal Tugimbe mkoani humo.

Amesema tamasha hilo litaambatana na uzinduzi wa filamu ya ‘Seven Days’ ambapo wataanza na usaili kwa wasanii watakaoshiriki katika tamthilia itakayo shutiwa jijini Mbeya.

”watu wangu wa Mbeya tukutane siku ya Idi Mosi katika tamasha la nyumbani festival litakalo fanyika katika ukumbi wa Royal Tugimbe na litaambatana na uzinduzi wa filamu ya Seveni Days” alisema Johari

Aidha mgeni rasmi katika tamasha hilo atakuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila pamoja na mkuu wa wilaya ya chunya Maryprisca Mahundi ambapo kabla ya hapo wataungana na majaji katika harambee maalumu.

Mbaroni kwa kukutwa na mafuta ya maiti ya binadamu
Njia za kuongeza mbegu za kiume

Comments

comments