Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya Simba John Bocco, leo jumatatu Februari 26-2018 amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18 kwa mwezi Januari na wadhamini wa ligi hiyo.

Kwenye kinyang’anyiro hicho Bocco aliwashinda nyota mwenzake wa Simba  Emmanuel Okwi na kiungo wa Mwadui FC Awesu Awesu

Nahodha huyo amekabidhiwa hundi ya sh milioni moja, ngao na kisimbuzi cha Azam TV kama sehemu ya zawadi hiyo.

Bocco alikabidhiwa zawadi hizo muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Mbao FC uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.

Nyota huyo wa zamani wa Azam FC amekuwa mchezaji wa pili wa Simba kupata tuzo hiyo baada ya Okwi aliyepata mwezi Agosti.

Shirikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT) lavunjwa
Video: Mtatiro adai serikali imetumia bilioni 10 kununua madiwani na wabunge