Nahodha na mshambuliaji wa kikosi cha Simba, John Bocco ‘Adebayor’ amesema historia inaonyesha wamekuwa na matokeo mazuri mbele ya timu za kiarabu na watafanya hivyo tena mbele ya Al Masry kesho.

Bocco ambaye anatarajiwa kuwa miongoni mwa nyota wa Simba watakaoshuka dimbani kesho amesema mchezo utakuwa mgumu na wanawaheshimu wapinzani wao lakini wamepinga kushinda.

Nyota huyo amesisitiza kuwa wachezaji watajitoa kwa asilimia mia kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika uwanja wa nyumbani ingawa amekiri haitakuwa kazi rahisi.

“Al Masry ni timu bora na ina wachezaji wazuri lakini bado historia inatubeba mbele ya timu kutoka nchi za Kiarabu, wachezaji tupo tayari kuitetea Simba.

“Hatukuwapa raha mashabiki wetu katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Stand United lakini kesho tutajitoa kuhakikisha tunafanikisha hili,” alisema Bocco.

Mwaka 2003 Simba ilifanikiwa kuwatoa mabingwa wa michuano ya klabu bingwa Afrika timu ya Zamalekh kutoka Misri.

Township Rollers yaibutua Young Africans Taifa
Pierre Lechantre: Nazifahamu mbinu za Al Masry