Ikiwa ni mwaka mmoja tangu mchezaji maarufu wa mieleka nchini Marekani, John Cena (40) kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake, Nikki Bella (32) ambaye naye ni mchezaji wa mieleka wawili hao wameamua kuvunja mahusiano yao kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

John Cena na aliyekuwa mpenzi wake wamedumu katika mahusiano kwa muda wa miaka sita mpaka hapo walipoamua kuvunja uhusiano huo na kila mmoja kuishi maisha yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa US Weekly umeripoti kuwa wawili hao wameachana na kufanya maamuzi hayo kuwa ya siri ili kuzingatia heshima ya kila mmoja.

” Ingawaje maamuzi haya ni magumu lakini tutaendelea kuheshimiana na kupendana kama zamani. Tumejadiliana kwa kina juu ya tukio hili la kuachana kwetu,” Wamesema wawili hao kwenye mahojiano na mtandao wa Weekly US.

Hata hivyo tetesi za wawili hao kuachana zilianza kusambaa mwezi uliopita lakini John Cena alinukuliwa akisema kuwa hawaongozani pamoja kwa sababu ambazo alieleza kuwa angezitaja baadae.

John Cena na mchumba wake walivalishana pete mnamo Aprili 2, mwaka jana.

Mwinyi alia na amani ya nchi
Mwanamke amshtaki Mariah Carey kwa kumnyanyasa kingono