Msanii kutoka Afrika ya kusini Sho Madjozi ambaye alipata nafasi ya ‘kuperfom’ katika kipindi cha television cha Kelly Crarkson (The clarkson show) ambapo mkali wa mieleka duniani John Cena alimfanyia suprize mwanadada huyo kitu ambacho hakutegemea kabisa.

Ikumbukwe september 30 John cena akiwa aktika show ya Ellen (The Ellen show) aliulizwa kuwa kuna msanii kutoka afrika ya kusini kaimba wimbo unaitwa John Cena ambapo alisema ndio anamfahamu na akamtaja jina anaitwa Sho Madjozi.

Kupitia ukurasa wa Tweeter wa Madzoji aliandika kuwa“Sikumuona akiingia kwa wakati huo watu walikuwa wakipiga kelele mimi ni kama ninlishtuka.”

Naye mkali huyo wa mieleka kupitia ukurasa wake wa tweeter aliposti picha akiwa na msanii huyo na kuandika kuwa ”Asante Kelly ClarksonTV kwa tukio kubwa na la kushangaza na ni heshima gani ya mimi kujifunza vitu vingi kutoka kwa Sho Madjozi hadithi na jinsi ilivyo lakini pia kwa kuona kuwa WWE inaweza kuhamasisha msanii kote ulimwenguni. wanasema “Fanya kilichobora uwe bora kwa sababu haujui ni nani anayeangalia au inamuthiri vipi”.

Madjozi anayetamba na wimbo wa John Cena wenye maneno kiswahili alisema kuwa hakuwahi kukutana na mcheza mieleka huyo japo alikuwa ‘akimtag’ staa huyo  kupitia mitandao ya kijamii bila ya  kupata mrejesho wowote.

”Mtaani kwetu hakukuwa na tv tulikuwa tunaangalia kwa watu  na moja kati ya vipindi ambavyo nilikuwa napenda kuviangalia ni mieleka na nilikuwa nampenda sana John Cena” alisema Madjozi.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 10, 2019
Yanga yajichotea fedha kwa mgongo wa Ndanda FC

Comments

comments