Mwimbaji John Legend amemrushia makombora mgombea anayeusaka urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump kwa njia tofauti na ile inayotumiwa na wasanii wengi wa Marekani hususan weusi.

Mwimbaji huyo wa ‘All of Me’ amewarusha wamarekani enzi za utumwa akifananisha wakati huo na kosa kubwa ambalo lilifanywa na watu waliogeuzwa kuwa watumwa na kwamba kosa hilo likifanywa na Wamarekani katika uchaguzi wa mwaka huu, Marekani itakuwa imejirudisha enzi za utumwa.

“Nadhani hata watu wa miaka ya 1800 hawakufikiria kama wao ni watu waovu bali waliwaruhusu taasisi ovu kuchukua nafasi na kudumu kwa muda mrefu,” John Legend aliiambia Variety TV.

“Tuko katika kipindi ambacho tuna mgombea mkubwa anayetaka kuingia ambaye amekuwa mbaguzi wa rangi anayetugawa katika hali zote. Ninataka kusema hayo wakati huu kwa sababu sitaki kudhani kama haiwezekani kwa nchi yetu kurudi nyuma katika kipindi kipindi kingine cha kuwa gizani,” alieleza.

Ingawa hakumtaja moja kwa moja, John Legend ambaye ametoa mtazamo wa kistaarabu limegeuka kuwa kombora la wazi kwa Donald Trump, mwanasiasa ambaye amezua sintofahamu hasa baada ya kuendelea kusisitiza kuwa Waislam hawatakiwi kuingia Marekani.

Tofauti na John Legend, wasanii wengi wamekuwa wakimporomoshea matusi Trump na kumkejeli kwa njia mbalimbali huku baadhi ya wananchi wakiingia barabarani kumpinga kwa nguvu kutokana na matamshi yake.

Video: Mkuu wa Mkoa DSM, Makonda amepokea milioni 100 kutoka CRDB
Video: Solo Thang amkingia kifua Jay Mo