Kiungo kutoka nchini Nigeria John Obi Mikel, amefanikiwa kuondoka Stamford Bridge na kuelekea mashariki ya mbali kujiunga na klabu ya Tianjin Teda inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini China.

Mikel amekamilisha mpango huo, baada ya kufanyiwa vipimo vya afya katika makao makuu ya klabu hiyo ambayo yapo kilomita 130 kutoka mji wa Beijing.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua na klabu ya Chelsea kwa zaidi ya muongo mmoja, ameondoka Stamford Bridge akiwa kama mchezaji huru kutokana na kutokua sehemu ya mipango ya meneja wa sasa Antonio Conte.

Obi amekubaliana na uongozi wa klabu Tianjin Teda kulipwa mshahara wa pauni 140,000 ambazo ni sawa dola za kimarekani 173,432 kwa juma.

Katika kipindi hiki cha majira ya baridi, klabu za China zimefanikisha usajili wa wachezaji kutoka barani Ulaya kama kiungo kutoka Serbia Nemanja Gudelj aliyejiunga na Tianjin akitokea Ajax Amsterdam, Oscar akitokea Chelsea pamoja na Carlos Tevez ambaye ametokea nchini kwao Argentina huko Amerika ya kusini.

Oscer amejiunga na klabu ya   Shanghai SIPG na Tevez amesajiliwa na Shanghai Shenhua.

Riyad Mahrez Mchezaji Bora Barani Afrika
Lowassa atajwa sababu ya deni la Milioni 1 mbele ya Mkuu wa Mkoa