Beki na nahodha wa klabu ya Chelsea, John Terry anategemewa kukataa ofa ya mamilioni ya Pauni zilizotangazwa na baadhi ya klabu za soka nchini China ambazo zinahitaji kujiimarisha, kwa kumnasa gwiji huyo.

Terry tangu jana amekua akiripotiwa kuwa kwenye mikakati ya baadhi ya klabu za nchini China, na tayari imethibitika aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Sven-Goran Eriksson amekuwa chagizo zuri kwa beki huyo ili akubali kujiunga na klabu anayoitumikia kwa sasa huko mashariki ya mbali ya Shanghai SIPG.

Naye aliyewahi kuwa meneja wa klabu ya Chelsea, Phil Scolari amekuwa akitumiwa na viongozi wa klabu ya Guangzhou Evergrande, ili kufanikisha safari ya Terry ya kutoka nchini England na kuhamia China.

Naye gwiji wa Stamford Bridge, Dan Petrescu ambaye ni meneja wa klabu ya Jiangsu Suning inayoshiriki ligi ya nchini China anatamani kufanya kazi na John Terry huku aliyekuwa mchezaji mwenzake Demba Ba akisisitiza kuwa tayari kumuona beki huyo akijiunga naye kwenye klabu za Shanghai Shenhua.

Hata hivyo taarifa za mapema hii leo zinaeleza kwamba Terry bado anahitaji kubaki Chelsea, kutokana na kuyazoea vyema mazingira ya klabu hiyo ambayo alianza kuitumikia tangu 1995 akisajiliwa kutoka West Ham Utd.

Meneja mpya wa klabu hiyo Antonio Conte, amekua na mazungumzo ya faragha na nahodha huyo ambayo mara nyingi hulenga suala la kumsisitiza abakie Stamford Bridge, huku akimuahidi ofa nono ambayo huenda ikamfanya akawa mchezaji atakaelipwa mshahara mkubwa klabuni hapo.

Terry's season is over after he was sent off against SunderlandJohn Terry akionyeshwa kadi ya njano iliyofuatiwa na nyekundu wakati wa mchezo wa ligi mwishoni mwa juma lililopita.

Terry kwa sasa kama ameshamaliza msimu wa 2015-16, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Sunderland, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mkataba wa beki huyo mwenye umri wa miaka 35, utafikia kikomo mwezi ujao na atakuwa huru kufanya maamuzi ya wapi atakapocheza soka lake msimu wa 2016-17 na kuendelea.

Danny Welbeck Kuzikosa Fainali Za Ulaya (Euro 2016)
Thomas Vermaelen Kusaidia Mipango Ya Kutetea Taji