Klabu ya Young Africans inatajwa kukamilisha mpango wa kumsajili Mlinda Lango wa klabu ya Aigle Noir ya Burundi Erick Johora.

Johora ambaye ni Mtanzania alikuwa sehemu ya kikosi cha Aigle Noir kilichotua nchini mwezi Agosti 2020 wakati wa maandalizi ya msimu 2020/21, na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Young Africans siku ya ‘MWANANCHI’.

Mlinda mlango huyo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans kitakachoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), itakayoanza Jumapili (Agosti Mosi) jijini Dar es salaam.

Usajili wa Johora, unadhihirisha wazi nafasi ya Malinda Lango mmoja wa Young Africans ataondolewa kwenye kikosi, hususan katika kipindi hiki cha usajili wa kuelekea msimu wa 2021/22.

Jina la Malinda Lango Metacha Mnata linatajwa huenda likakatwa kwenye orodha ya wachezaji watakaosajiliwa klabuni hapo kwa ajili ya msimu ujao, kutokana na zoezi la kusaini mkataba mpya kushindikana.

Rais Mwinyi afanya uteuzi
Nugaz: Sikulala siku tatu, nililazwa hospitali