Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ametoa salamu za shukrani kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, alipokuwa awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate ameandika, “Kwanza, kwa unyenyekevu mkubwa namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutupatia sote zawadi ya uhai.

Pili, kwa namna ya kipekee, ninamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu, Mhe. @samia_suluhu_hassan kwa kuendelea kuniamini na kunipa nafasi ya kumuwakilisha na kutoa mchango wangu wa kuwatumikia Watanzania wenzangu na WanaTemeke kupitia majukumu ya Ukuu wa Wilaya.

Tatu, Shukrani zangu nyingi kwa Viongozi, Watendaji, na Wananchi wenzangu wa Wilaya ya Kisarawe. Kwa mashauri na ushirikiano mzuri kwa kipindi chote tulichokuwa tukihudumu pamoja, kupitia umoja na mshikamano wetu tulifanikisha mengi na kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zinaikabili Wilaya ya Kisarawe.

Nne, kwa upande wa Wananchi wenzangu wa Temeke, Viongozi na Watendaji wote, ninawasihi na kuwaomba ushirikiano wenu. Mimi ninawaahidi Utumishi wa pamoja na uliotukuka kwa manufaa ya Temeke yetu. Lengo letu kubwa liwe kuiona Temeke inayofanya vizuri zaidi kuanzia pale mlipopafikisha wezangu katika Sekta ya Elimu, Afya, Michezo, Biashara na Uwekezaji, Usafiri wa Umma, Sanaa, fursa za Ajira, usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.

Mwisho, ninawashukuru sana Ndugu, Jamaa, Marafiki, na Wote kwa pongezi zenu na kunitakia kheri kwenye kituo changu kipya cha UTUMISHI.
Ahsanteni tena. #KaziIendelee #TemekeKwanza,” ameandika Jokate.

Jokate aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Rais Samia Suluhu Hassan, Jumamosi, Juni 19, 2021 ambapo kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe tangu alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tano wa Tanzania, Hayati Dkt John Magufuli, Julai 28, 2018.

Waliodhaniwa kubeba msiba wasababisha ajali
Man Utd kuibomoa Borussia Dortmund