Mwanamitindo maarufu, ambaye pia ni Kaimu katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo (Kidoti), amesema kwa sasa hana mamlaka ya kumuongelea mwanaume yeyote mwenye mahusiano ya kimapenzi na yeye mpaka atakapopata mwanaume wa kumuheshimu na  kumuoa.

”Sipo tayari kuzungumzia maisha yangu ya kimapenzi hadi nitakapopata mwanaume atakayeniheshimu na kunioa, huyo ndiye nitakuwa na mamlaka ya kumzungumzia”.

Kidoti ni mwanamke anayetambulika kama malkia wa nguvu, ni mmiliki wa kampuni ya kidoti inayojishughulisha na aina tofauti za nywele ikiwemo rasta, vibanio na sasa vifaa vya mashuleni.

Amesema Kidoti, ”Baada ya nywele na vibanio sasa naleta vifaa vya shule kwa wanafunzi ikiwemo madaftari, kompasi, rula pamoja na mabegi ya shule na vitakuwa na nembo ya kidoti, lengo ni kuongeza wigo wa bidhaa kwa wanafunzi na kuongeza ajira kwa vijana,”

Video: Muhongo afunguka mkataba madini, Mali za vinara wa Escrow zakamatwa
Jopo la Congress lamuweka kitimoto Trump, lataka atoe vielelezo