Kiungo Mkongwe wa Klabu ya Simba SC Jonas Mkude ameupongeza Uongozi wa Klabu hiyo kwa kufanikisha kumpata Kocha Zoran Maki, aliyerithi mikoba ya Kocha kutoka nchini Hispania Franco Pablo Martin.

Zoran Maki alitangazwa kuwa Kocha Mkuu Simba SC mwezi Juni mwaka huu, baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumsaka Kocha Mpya klabuni hapo, uliochukua zaidi ya mwezi mmoja.

Mkude amesema Kocha huyo kutoka nchini Serbia amekua kama mzaizi kwa wachezaji, kutokana na maelekezo anayoyatoa wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya 2022/23, nchini Misri.

Amesema Uongozi umefanya kazi kubwa ya kumpata kocha kama Zoran, na wao kama wachezaji wanajivunia kuwa na kocha huyo ambaye aliwahi kufanya kazi katika vilabu vikubwa barani Afrika.

“Niupongeze uongozi wa Simba SC, umetuletea kocha mzuri, ni kama mzazi kwetu kwa sababu anaishi na sisi vizuri na kutuelekeza pale tunapokosea, hachoki kufanya hivyo kwa sababu lengo lake nikutuona tukifanya anachokita hadi tupatie,”

“Tumekua na maandalizi mazuri tangu tulipofika hapa Ismailia-Misri, Kocha anatupa mazoezi yanayotujenga, kila mmoja wetu anaona tunapoelekea kama timu, nina imani Kocha Zoran ana jambo kubwa ambalo litaweza kuwapa furaha mashabiki wa Simba SC msimu ujao.”

“Sisi wachezaji tuna deni kubwa sana kwake kama Kocha, tunatakiwa kupambana ili kukamilisha makubaliano yaliopo kati yake na Uongozi ili kuifikisha timu pale inapohitaji kufika, hata mashabiki nao watakua na mchango wao katika hili.” amesema Mkude.

Kabla ya kuajiriwa Simba SC, Kocha Zoran alikuwa Kocha Mkuu wa kikosi cha klabu ya Al-Tai, ambapo hapo kabla pia alifundisha klabu ya CR Belouzdad ya Algeria.

Pia kocha huyo anayesfika kwa soka la kushambulia kwa kasi na kujihami kwa pamoja, alizifudnisha klabu za Al-Hilal ya Sudani, Moghreb Tetouan, Wydad Casablanca ya Morocco pamoja na Sagrada ya Angola.

Uchaguzi wa Kenya: Jaribio jingine la Kidemokrasia
Juma Pondamali: Taifa Stars inakwenda kumaliza