Kiungo na nahodha wa klabu ya Liverpool Jordan Henderson amempigia chepuo kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate, kwa kuwataka viongozi wa chama cha soka FA, kumpa ajira ya kudumu.

Henderson ambaye aliwaongoza wenzake kama nahodha wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya Slovenia, amesema Southgate ameonyesha kuwa na vigezo vyote vya kukiongoza kikosi cha timu yao ya taifa, hivyo haoni sababu kwa viongozi wa FA kuendelea na mchakato wa kumsaka kocha mwingine.

Amesema matokeo ya michezo waliyocheza tangu kocha huyo wa muda alipoingia madarakani kuchukua nafasi ya Sam Allardyce, yamekuwa na mtazamo chanya kwake kama mchezaji na anaamini endapo ombi lake litakubalia Southgate atakua na nafasi kubwa ya kufikia lengo la uipelekea Uingereza kwenye fainali za kombe la dunia zitakazochezwa nchini Urusi mwaka 2018.

Image result for Jordan Henderson and Gareth Southgate on sky sportsJordan Henderson

“Kocha amekuwa na ushirikiano mzuri dhidi yetu tangu tulipokua kambini tukiajiandaa na michezo miwili tuliyocheza, na kila mmoja alionyesha kufurahia kilichotendeka katika uwanja wa mazoezi hadi kwenye uwanja wa mapambano,”

“Tunatakiwa kuendelea kuwa na Southgate kwa maslahi ya taifa, uwepo wake kama kocha umeonyesha tofauti kubwa ya kujituma kwa timu yote kwa ujumla na ndio maana tuliweza kushinda mchezo dhidi ya Malta kwa mabao mawili na kisha kutoka sare dhidi ya Slovenia.” Alisema Henderson mwenye umri wa miaka 26.

Southgate, mwenye umri wa miaka 46, bado anatambuliwa na FA kama kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Uingereza na kuteuliwa kwake kushika nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi la timu ya wakubwa kwa muda, kulisababishwa na maamuzi ya kujiuzulu kwa Sam Allardyce mwezi uliopita, baada ya kufichua siri za chama cha soka.

Vincenzo Montella Amkataa Cesc Fabregas AC Milan
Real Madrid Kuweka Vizuizi Kwa Bale, Ronaldo, Pepe Na Modric