Mlinda mlango kinda kutoka England, Jordan Pickford amekamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Everton akitokea klabu iliyoshuka daraja ya Sunderland kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 30.

Pickford mwenye umri wa miaka 23, amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kufuzu vipimo vya afya usiku wa kuamkia leo.

Usajili huo unamfanya Pickford kuwa mlinda mlango ghali zaidi kwa upande walinda mlango raia wa England.

Pia unakua mlinda mlango wa tatu ghali zaidi dunia nyuma ya Ederson Moraes wa Manchester City aliyenunuliwa kwa Pauni milioni 34.7 na Gianluigi Buffon wa Juventus aliyenunuliwa kwa Pauni milioni 32.6.

Leicester City Washinda Vita Ya Harry Maguire
Gianluigi Donnarumma Ajiweka Sokoni

Comments

comments