Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina Jorge Sampaoli ametangaza kikosi cha wachezjai 35, ambacho kitaingia kambini kujiandaa na fainali za kombe la dunia zitakazoanza Urisi Juni 14.

Sampaoli ametangaza kikosi hicho, huku akitarajia kuwatema wachezaji kumi, na kusaliwa na wachezaji 25 ambao atasafiri nao hadi nchini Urusi tayari fainali hizo.

Kwa sasa kikosi hicho kilichomjumuisha Lionel Messi, Paulo Dybala na Mauro Icardi kitafanya maandalizi kwa pamoja sambamba na kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki, hali ambayo itamuwezesha kocha Sampaoli kuteua watakaofikia malengo yake, kabla ya safari ya Urusi.

Kikosi cha Argentina kilichotangazwa na kocha Sampaoli hii leo upande wa Makipa ni Sergio Romero, Wilfredo Caballero, Nahuel Guzmán, Franco Armani.

Mabeki: Eduardo Salvio, Gabriel Mercado, Nicolás Otamendi, Javier Mascherano, Federico Fazio, Marcos Rojo, Marcos Acuña, Nicolás Tagliafico, Ramiro unes Mori, Germán Pezzella, Cristian Ansaldi.

 Viungo: Lucas Biglia, Ever Banega, Giovani Lo Celso, Manuel Lanzini, Enzo Pérez, Pablo Pérez, Leandro Paredes, Guido Pizarro, Rodrigo Battaglia, Ricardo Centurión, Ángel Di María, Diego Perotti, Maximiliano Meza, Cristian Pavón .

 Washambuliaji: Paulo Dybala, Sergio Agüero, Gonzalo Higuaín, Lionel Messi, Mauro Icardi, Lautaro Martínez.

Alex Iwobi, Victor Moses kuongoza jahazi la Super Eagle
Thomas Tuchel Boss Mpya Paris Saint-Germain

Comments

comments