Klabu ya West Ham Utd ipo katika harakati za kuisaka saini ya beki wa kati kutoka nchini Ureno na klabu ya Southampton Jose Fonte, kwa dau la Pauni milioni 10.

SunSport wameripoti kuwa, juma lililopita The Hammers walituma ofa ya Pauni milioni 4 kwa ajili ya kushawishi usajili wa beki huyo, lakini uongozi wa The Saint uliikataa kwa kigezo cha ofa hiyo kutokau na uzito wa thamani ya mchezaji huyo.

Mapema hii leo kituo cha televisheni cha Sky Sports kimeripoti kuwa, tayari viongozi wa West Ham Utd wamerekebisha ombi lao la usajili, na wanajiandaa kuanza kufanya mazungumzo ya usajili wa Fonte.

Meneja wa West Ham Utd Slaven Bilic, anaamini endapo atafanikiwa kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa ameiboresha safu yake ya ulinzi ambayo kwa sasa ina wachezaji kama Winston Reid, Angelo Ogbonna pamoja n James Collins huku akilazimisha kumtumia kiungo Cheikou Kouyate kama beki wa kati wakati inapohitajika.

Fonte ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilichotwaa ubingwa wa Euro 2016, aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka Southampton mwanzoni mwa mwezi huu kwa kigezo cha kutaka kucheza katika mazingira mapya yatakayompa ushindani.

Alijiunga na klabu ya Southampton akitokea Crystal Palace, Januari 2010.

Aliisaidia The Saint kupanda daraja misimu minne iliyopita na tayari ameshaitumikia klabu hiyo katika michezo 286.

Sheria Za Soka Mbioni Kubadilishwa
Video: Waziri Nape aeleza kusikitishwa na shutuma kuhusu bidhaa feki za wasanii