Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho amesema alitambua kikosi chake kilikua hatarini kuondolewa kwenye michuano ya kombe la ligi (Carabao Cup) dhidi ya Derby County, baada ya kuona matayarisho ya upigaji wa penati ya beki Phil Jones.

Beki huyo alikosa mkwaju wa penati ya nane, katika mchezo huo na kuiwezesha Derby County kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwa ushindi wa penati nane kwa saba, kufuatia matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili yaliyopatikana katika muda wa kawaida (Dakika 90).

Mkwaju wa beki huyo uliokolewa na mlinda mlango wa Derby County Scott Carson.

Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, Mourinho alisema mara zote Jones anapokua katika mazoezi ya kupiga penati kuna hatua kadhaa huzichukua, na anapoziona huamini anakosa, na ndivyo ilivyotokea katika mchezo huo wa jana uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Amesema wachezaji ambao humpa wakati mgumu katika zoezi la upigaji wa penati ni Jones na Eric Bailly, ambaye hata hivyo jana alifanikiwa kupata mkwaju wake.

“Tumekua tukifanya mazoezi ya kupiga penati mara kwa mara, kuna baadhi ya hatua huwa naziona na kwa wachezaji hawa wawili, lakini kwa Jones, imekua kama mazoea kwake, na nilipoona amefanya moja ya hatua hizo niliamini tupo kwenye hatari ya kuondolewa kwenye michuano hii,” Mourinho aliwaambia waandishi wa habari.

“Nimekubaliana na matokeo, ninawapongeza Derby County kwa ushindi walioupata na ninawatakia kila la kheri kwenye michezo yao inayokuja ya michuano hii ya kombe la ligi.”

Kwa upande wa meneja wa Derby County Frank Lampard, ambaye aikua mchezaji wa Mourinho wakati akiwa na kikosi cha Chelsea, amesema ilikua kama bahati kwake kufanikisha ushindi dhidi ya bosi wake wa zamani.

“Nilishangaa na kushtushwa kwa kilichotokea, sikuamini kama ningeweza kuuvuka mtihani huu, ukicheza dhidi ya Mourinho unapaswa kujiandaa kwa kila hali, ninamshukuru mungu nimefanikiwa, kikosi changu kimeonyesha soka safi lililotupa ushindi.” Alisema Lampard.

“Ni vuguu kushinda katika uwanja wa Old Trafford, ni mara yangu ya kwanza kuja hapa kama meneja na kufanikisha jambo hili, sina budi kuwapongeza wachezaji wangu kwa hatua nzuri waliyoifikia, na tupo tayari kuendelea kupambana.”

Wakati Derby County wakiivurumisha Man Utd kwa ushindi wa penati nane kwa saba, matokeo ya michezo mingine yalikua kama ifuatavyo.

AFC Bournemouth 3 – 2 Blackburn Rovers

Blackpool 2 – 0 Queens Park Rangers

Burton Albion 2 – 1 Burnley

Millwall 1 – 3 Fulham

Oxford United 0 – 3 Manchester City

Preston North End 2 – 2 Middlesbrough (Middlesbrough ameshinda kwa penati 4 kwa 3)

Wolverhampton Wanderers 0 – 0 Leicester City (Leicester City ameshinda kwa penati 3 kwa 1)

Wycombe Wanderers 3 – 4 Norwich City

West Bromwich Albion 0 – 3 Crystal Palace

Leo michuano hiyo inaendelea tena kwa michezo mingine kuchezwa.

Arsenal Vs Brentford

Liverpool Vs Chelsea

Nottingham Forest Vs Stoke City

West Ham United Vs Macclesfield Town

Tottenham Hotspur Vs Watford

Lionel Messi, Cristiano Ronaldo wamtibua Fabio Capello
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine wizara ya mambo ya nje