Ligi kuu ya soka nchini Uingereza itaendelea tena hii leo kwa mchezo  mmoja kupigwa kwenye uwanja wa Anfield kati ya wenyeji Liverpool dhidi ya Man Utd.

Mchezo huo ambao unawakutanisha mahasimu wa soka la Uingereza unasubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na uwepo wa meneja wa Man Utd Jose Mourinho ambaye atakua akielekea Anfield kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi cha Mashetani wekundu ambao ni maadui wakubwa wa Liverpool.

Mchezo huo ambao utachezwa mishale ya saa nne usiku kwa saa za Afrika mashariki, tayari umeshagubikwa na figisu figisu za muamuzi Anthon Taylor ambaye amepewa jukumu la kusimamia sheria 17.

Mashabiki wa Liverpool wanaamini Taylor atakua na sababu zote za kuibeba Man Utd kutokana na kuwa mzaliwa wa mji wa Manchester na mpaka sasa ni makazi wa mji huo tena nyumba yake ipo umbali wa maili sita kutoka kwenye uwanja wa Old Trafford.

Kwa upande wa meneja wa Man Utd Jose Mourinho amesema muamuzi huyo mwenye umri wa miaka 37, amepoteza sifa za kuchezesha mchezo wa hii litokana presha kubwa iliyotengenezwa na mashabiki wa pande zote mbili kwa kuamini huenda mmoja utanyongwa kwa makusudi.

Amesema hali hiyo huenda ikachangia kumuondoa Taylor katika uweledi wa kuchezesha soka safi na lenye kuvutia, hivyo amekitaka chama cha soka nchini Uingereza FA kufikiria upya maamuzi waliyoyachukua ya kumtangaza muamuzi huyo.

Liverpool watamkosa mshambuliaji wao wa pembeni Adam Lallana ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyonga, Georginio Wijnaldum anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Beki wa pembeni Nathaniel Clyne pamoja na Dejan Lovren wanatarajiwa kurejea kikosini kufuatia vipimo kuonyesha wana utimamu wa mwili huku Emre Can akipewa nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool kwa mara ya kwanza msimu huu.

Kwa upande wa Man Utd, Henrikh Mkhitaryan pamoja na beki Luke Shaw wameripotiwa kuwa na utimamu wa mwili hivyo wana nafasi kubwa ya kucheza lakini Mourinho ataendelea kumkosa Phil Jones.

Arsene Wenger: Mesut Ozil Bado Ana Ndoto Za Kuitumikia Arsenal
Waziri Makamba awataka Wafugaji na Wakulima Kuunda Kamati ya Amani