Meneja wa klabu bingwa nchini England, Chelsea, Jose Mourinho amefunguliwa mashtaka na chama cha soka nchini humo FA, kutokana na kauli aliyoitoa mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, ambapo The Blues walikubali kufungwa nyumbani Stamford Bridge mabao matatu kwa moja dhidi ya Southampton.

FA, imemtuhumu Mourinho kwa kudai alitoa kauli chafu dhidi ya muamuzi Robert Madley, kwa kusema alionyesha upendeleo ulio dhahir dhidi ya Southampton kwa kushindwa kuizawadia penati Chelsea katika mchezo huo.

Mourinho alisema kulikua na msukumo wa kimakusudi wa kukiangamiza kikosi chake katika mchezo huo, na muamuzi huyo huenda alishirikiana na wasaidi wake kutimiza azma waliyoingia nayo uwanjani.

FA, wamempa muda meneja huyo kutoka nchini Ureno mwenye umri wa miaka 52, hadi Oktoba 8, kujibu mashtaka yanayomkabili na kama itakua kinyume na hapo sheria za kinidhamu zitatumika dhidi yake.

Chelsea, walipoteza mchezo wanne mwishoni mwa juma lililopita na kuendelea kujiweka katika mazingira magumu ya kuanza vyema msimu huu, hasa ikizingatiwa wao ndio mabingwa watetezi.

Lowassa: Mlitaka nife… Tupo na Tupo Hai
Rodgers Aondoka Kwa Kuacha ujumbe Mzito