Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho amefungiwa mchezo mmoja pamoja na kutozwa faini ya Pauni elfu nane (8000), kufuatia kosa la kutoa maneno makali dhidi ya waamuzi waliochezesha mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Burnley.

Kamati ya nidhamu ya chama cha soka nachini England FA, imetangaza hukumu kwa meneja huyo baada ya kukubali mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake siku mbili zilizopita.

Mourinho alipewa muda hadi ijumaa jioni, ili awasilishe utetezi wa kupinga mashtaka yaliyokua yakimkabili, lakini hakufanya hivyo na badala yake alikubali, jambo ambalo liliipa idhini kamati hiyo kuendelea na shughuli za kutoa hukumu.

Kwa mantiki hiyo, Mourinho hatokua sehemu ya benchi la ufundi la Man Utd katika mchezo wa ligi ya nchini England mwishoni mwa juma hili, ambapo kikosi cha Mashetani wekundu kitakua ugenini Liberty Stadium kikicheza dhidi ya Swansea City.

Katika hatua nyingine Mourinho ametozwa faini ya Pauni elfu hamsini (50,000), kufuatia kosa la kutoa kauli ya kushurutisha mwamuzi Anthon Taylor aliyechezesha mchezo kati ya Man Utd dhidi ya Liverpool Oktoba 17, abadilishwe kwa kutumia kigezo cha shinikizo ambalo lilikua likiendelea baina ya mashabiki wa klabu hizo mbili kwenye mitandao uya kijamii.

Thomas Tuchel: Sikumpanga Aubameyang Kwa Sababu Binafsi
Mtifuano Wa Ulaya Washika Kasi, Real Madrid Wabanwa