Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anajiapanga kuvuga mipango ya klabu bingwa nchini Italia Juventus, kwa kuanza kumshawishi kiungo Javier Alejandro Mascherano ajiunge nae huko Old Trafford.

Mascherano anatajwa kufikia pazuri na uongozi wa klabu ya Juventus, kwa kukubali baadhi ya masuala binafsi, kabla ya FC Barcelona kufanya biashara na kumruhusu kuondoka.

Mourinho anahusishwa kuwa katika mawindo ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, saa chache baada ya kuthibitishwa mbele ya waandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita.

Hata hivyo Mascherano, anatarajiwa kutoa maamuzi ya mwisho ya kuafiki ama kukataa kimaandishi makubaliano binafsi na uongozi wa Juventus hii leo, na kama atashindwa kufanya hivyo itaonyesha dhahir mipango ya Mourinho ya kuingilia dili hilo imefanikiwa.

Juventus wapo tayari kutoa kiasi cha Euro milion 80, kama ada ya usajili wa Mascherano, kiasi ambacho bado kinaweza kutolewa na Man Utd.

Gharama za mchezaji huyo kwa mwaka ambazo amekua akizipata akiwa na FC Barcelona ni Euro milion 7 kwa mwaka, ambazo bado Man utd wana uwezo wa kumtimizia.

Hector Bellerin, Juanfran Kuwania Nafasi Kikosi Cha Hispania
N'Golo Kante Azichimba Mkwara Arsenal, PSG