Baada ya kipigo cha kushangaza kutoka kwa Bernoumoth cha goli 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge, kocha Jose Mourinho wa Chelsea ameitoa Chelsea katika kuwania nafasi nne za juu huku akisisitiza kuwa wanahitaji kupigana kwa ajili ya nafasi sita za juu.

Jose amesema kuwa kabla ya mchezo huo walikua na imani na mipango ya kugombana kuingia top 4 baada ya awali kujitoa katika mbio za ubingwa, na sasa anasema top 6 ndio kitu pekee wanahitaji kugombania kama timu.

Mourinho anasema kama timu walishambulia sana huku kila mmoja akiwa anasubiria kuona goli lakini badala yake Bernoumoth wakapata bao katika dakika za mwisho za mchezo, katika mechi ambayo Mourinho amemtupia lawama mwamuzi kwamba aliwanyima penalti.

Kuhusu usajili wa wachezaji wapya mwezi Januari, Mourinho anasema haoni kama anastahili kuomba pesa za kununua wachezaji kutokana na fomu mbaya ya timu yake msimu huu, huku akisema kuwa jukumu sio la viongozi kutoa pesa za usajili bali wachezaji waliopo kujitolea kuinusuru klabu yao.

Jose anasema wana washambuliaji wazuri chini ya Diego Costa na Loic Remmy kwani msimu iliopita walionesha kwa kufunga mabao mengi. Lakini Mourinho akasema tatizo lililopo ni kwamba hawafungi hivi sasa huku Chelsea ikiwa haijafunga goli katika mechi tatu mfululizo.

Chelsea sasa wanashika nafasi ya 14 wakiwa na points 3 tofauti na mstari wa kushuka daraja, na kuachwa points 17 na kinara wa ligi Leicester City, lakini Mourinho anawatoa hofu mashabiki wake kwamba Chelsea haitoshuka daraja.

Kuelekea Disemba 12, Yanga Bado Hakijaeleweka
Magufuli aitumbua Bandari, Amsimamisha Katibu Mkuu, Avunja Bodi na Kutimua maafisa