Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho amejitetea katika mkutano na waandishi wa habari, baada ya kikosi chake kupokea kisago cha mabao matatu kwa sifuri kilichotolewa na Tottenham Hotspurs usiku wa kuamkia leo.

Mourinho alianza kujitetea katika mkutano na waandishi wa habari kwa hasira, baada ya kuulizwa swali kuhusu mfumo anaoutumia, ambao unadhaniwa kuwa chanzo cha kupoteza mpambano huo uliokua unasubiriwa na mashabiki lukuki duniani kote.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, alikiri kupoteza mchezo lakini akaonyesha kudharau swali aliloulizwa na waandishi wa habari, na badala yake akajitetea kwa kusema yeye ndio meneja pekee alietwaa ubingwa wa England mara nyingi kuliko mameneja wengine katika ligi hiyo kwa msimu huu.

‘Msimu uliopita tulipoteza hapa (Old Trafford)  dhidi ya Sevilla na kila mtu alituzomea, kwa sababu tulistahili, ninaamini kikosi kwa wakati ule hakikua kizuri na kilipaswa kupoteza”

‘Leo (Jana) wachezaji wameondoka uwanjani wakiwa wamepoteza mchezo, lakini mashabiki wamewapigia makofi, kwa sababu wamestahili. Hivyo endelea kujaribu na ujaribu, kujaribu ili ujaribu.

‘Nimemaliza… unajua nini, nini maana ya kupoteza kwa kufungwa mabao matatu? 3-0. 3-0. Unajua maana yake [huku akionyesha videlo vitatu vya mkono wake wa kulia]. 3-0.

‘Hii inamaanisha mataji matatu ya ligi ya England (Premierships), nimetwaa mataji mengi dhidi ya mameneja wengine 19 katika ligi hii msimu huu. Mataji matatu kwangu na mawili kwao. Heshimu, heshimu, heshimu, heshimu.’

Video: Makonda amalizwa, Upinzani watabiriwa kufa
Video: Manchester United yachakazwa bao 3- 0 na Spurs