Meneja mpya wa Man Utd Jose Mourinho amempendekeza aliyekua beki wa klabu hiyo Rio Ferdinand katika orodha ya watu anaotaka kufanya nao kazi kwenye benchi la Ufundi katika mapinduzi yake Manchester United.

Mourinho alitangazwa kumrithi Mholanzi Louis van Gaal Ijumaa akienda na masahiba zake anaaowaamini Rui Faria na Silvino Louro katika zama mpya Old Trafford.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, anataka Ferdinand awe mmoja wa makocha wake Wasaidizi katika benchi imara la Ufundi Man United.

Kuna wasiwasi juu ya mustakabali wa Ryan Giggs, ambaye anatarajiwa kuwa na mazungumzo na bosi wake mpya akirejea kutoka mapumzikoni Dubai.

Mourinho anaelekea kutaka kuwabakiza watu ambao wanaijua vizuri Man United na ni matumaini Giggs ataendelea na kazi yake hiyo ya muda mrefu sasa, ambayo ni daraja kati ya timu ya vijana ya 21 na kikosi cha kwanza.

Hiyo inatarajiwa pia kwa Ferdinand, ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 12 akishinda mataji sita ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya=.

Ferdinand, ambaye anaendelea na masomo ya ukocha kwa sasa, atakuwa na maamuzi atakapopelekewa ofa ya kufundisha United kuikubali au kuamua kutulia familia yake changa nyumbani kwaje, Kusini Mashariki.

Rio ana watoto watatu alioachiwa na mkewe, Rebecca aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa mwaka jana.

Juuko Murshid Asafiri Na Kikosi Cha Uganda Kuelekea Kusini
Kocha wa Pacquiao atosa ombi la Mayweather licha ya kumtamanisha kwa mamilioni