Meneja wa Manchester Manchester United  Jose Mourinho amepanga kuboresha safu ya kiungo ya timu hiyo kwa kumsajili Marco Verratti toka Paris Saint Germain.

Gazeti la Italia Outlet Corriere Dello Sport limeripoti kuwa  United wanajiandaa kutoa dau nono la pauni milioni 79 kwa kupata huduma ya kiungo huyo.

Verratti mwenye umri wa miaka 23 ni rafiki mkubwa wa  Zlatan Ibrahimovic ambaye naye anahusishwa kujiunga na Mashetani hao baada ya Juni 30 atakapo maliza mkataba wake na PSG.

Mabingwa hao wa Ufaransa ambao wana pesa za kutosha wanaonekana kutokuwa tayari kumuachia kiungo huyo kutokana na kuona ugumu wa kupata mrithi wake atakayeweza kuziba pengo lake akitimkia United.

Verratti amekuwa katika kiwango bora msimu huu kiasi cha kuvutia klabu kubwa barani Ulaya ambao wameonesha nia ya kutaka kumsajili kuongeza nguvu katika vikosi vyao.

Verratti alijiunga na  PSG akitokea Pescara ya Italia mwaka  2012 kwa ada ya pauni 9.5 milioni na kugeuka mchezaji muhimu kwa wababe hao wa Ufaransa.

Mkataba wake na wababe hao wa Ufaransa unamalizika mwaka 2020 na kuna kipengele cha kuongezeka zaidi kulingana na kiwango cha mchezaji ambaye alishindwa kusafiri na kikosi cha Azzuri kinachoshiriki Euro nchini Ufaransa kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Stand Utd Kufanya Uchaguzi Wa Viongozi Juni 26
Didier Kavumbagu Awapa Masharti Magumu Mbeya City