Viungo Paul Pogba na Marouane Fellaini hawatocheza mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la ligi (EFL Cup), ambapo Man Utd watawakabili wagonga nyundo kutoka jijini London West Ham Utd siku ya jumatano.

Viungo hao wawili walionyeshwa kadi za njano katika mchezo wa ligi ya England uliochezwa jana kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya West Ham Utd, ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Makosa waliyoyafanya katika mchezo huo, yamewasababishia wachezaji hao kufikisha kadi tano za njano kila mmoja, ambapo kisheria wanapaswa kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja wa michuano ambayo ipo chini ya chama cha soka nchini England FA.

Kukosekana kwa Pogba na Fellaini huenda likawa pigo kubwa kwa meneja Jose Mourinho, ambaye anatamani kuona kikosi chake kikisonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England.

Ricardo Kaka Asaka Heshima Orlando City
Bodi ya mikopo yadaiwa bilioni 1.7