Mpango wa Manchester United wa kutaka kumsajili beki wa kati kutoka nchini Ivory Coast na klabu ya Villarreal, Eric Bailly zimeungwa mkono na kupewa baraka na mtu wa karibu na beki huyo.

Meneja mpya wa Man Utd, Jose Mourinho mwishoni mwa juma lililopita, alianzwa kuhusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Bailly mwenye umri wa miaka 22, kwa ada ya usajili ya Pauni milion 31.

Kocha wa kikosi cha pili cha Espanyol, Manolo Marquez, amekuwa mtu wa kwanza kumpongeza Mourinho katika harakatiu zake za kutaka kumsajili beki huyo kwa kusema atafanya jambo lenye manufaa kama atakamilisha kumsajili Bailly.

Marquez, ambaye alimuendeleza kisoka Bailly amesema beki huyo amekuwa muhimili mkubwa katika klabu ya Villarreal na uwezo wake utasaidia harakati za meneja huyo kutoka nchini Ureno, za kutaka kuona Man Utd inarejea katika heshima ya kutwaa mataji.

Marquez akaenda mbali zaidi kwa kusema Bailly amekua na vigezo vya kucheza kwa umakini anapokua uwanjani na wakati mwingine humfananisha na nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos.

“Nina wajibu wa kusema chochote kuhusu Bailly kwa sababu ninamfahamu tangu akiwa kijana mdogo, na ninaamini kama atasajiliwa na Man utd, itakua ni vyema kutokana na uwezo na umakini alionao mchezaji huyo,”

“Bailly anataka kushabihiana na Sergio Ramos na kama ataelekea England kila mmoja atafurahishwa na kiwango chake, kwa sababu Man utd inahitaji kuwa na beki makini kama huyu,”

“Nilishtushwa na taarifa za mpango wa Jose Mourinho wa kutaka kumsajili Bailly lakini baadae niliamini uwezo na ujasiri wake ndio chanzo cha kuwa sehemu ya mkakati wa meneja huyo bora duniani.” Alisema Marquez al;ipokua anahojiwa na mwandidhi wa mtandao wa ESPN.

Borussia Dortmund kuachana Rasmi Na Henrik Mkhitaryan
Wanafunzi kuhukumiwa hadi miaka 10 jela kwa kuharibu picha ya Rais