Kocha  wa Manchester United Jose Mourinho amesema haamini kama atastaafu kazi ya ukocha akiwa bado katika klabu hiyo ya Uingereza.

Huu ni msimu wa pili kwa Mourinho mwenye umri wa miaka 54 akiwa kocha wa Man Utd na bado ana mkataba na klabu hiyo lakini ikumbukwe kuwa kocha huyo hajawahi kukaa zaidi ya miaka minne katika klabu moja, mpaka sasa amefanya kazi katika jumla ya klabu saba.

Akiongea na kituo kimoja cha Televisheni nchini Ufaransa Mourinho alisema anafikiri kwamba Paris St-Germain ni klabu nzuri sana yenye wachezaji bora, kauli iliyozua maswali iwapo kocha huyo atahamia PSG siku za mbeleni.

“Mimi bado ni kocha anayepatwa na wasiwasi, mwenye ndoto, na mwenye hamu ya kufanya mambo mapya,” alisema Mourinho.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Fc Porto alikiambia kipindi cha Telefoot cha TF1 kwamba hana uhakika kama atamaliza kazi ya ukocha akiwa Man Utd.

“Kwa nini Paris? Kwa sababu kuna jambo maalum huko. Ustadi, ubora, ujana, mambo mazuri sana,” aliongeza Mourinho.

Kauli hizi za Mourinho huenda zikawa za kutaka kuwapa presha Manchester United ili wampe mkataba mwingine wa muda mrefu.

 

Nakumatt ya Mlimani City yafungwa
Majaliwa awapa somo mawaziri walioteuliwa