Jose Mourinho amewapiga dongo mashabiki wa Liverpool kwa kuwaambia walidhani huenda mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ungekua rahisi kwao na kumaliza wakiwa na point tatu muhimu.

Mourinho alietupa dongo hilo kwa mashabiki wa soka wa Liverpool kwa kuamini matokeo ya sare ya bila kufungana yamewafunga mdomo, na kuwapotezea matarajio yao mengi waliokua wamejiwekea ya kuhakikisha wanakua na furaha mwishoni mwa dakika 90.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, alidai kuwa huenda kila shabiki wa Liverpool aliamini kikosi cha Man Utd kilikwenda Anfield na matarajio ya kupoteza, na ndio maana matumaini yao yalikua juu.

Hata hivyo Mourinho alikiri matokeo yaliyopatikana yanakubalika kitaalamu kutokana na hali ya mchezo ilivyokua, na anaamini wapinzani wao walikua kwenye hali ya kupambana, lakini umakini wa kikosi chake uliweza kuzuia mipango ya wenyeji.

“Ulikua mchezao mgumu sana kwetu na kwao pia,” Alisema Mourinho. “Lakini naamini ulikua mgumu zaidi kwa upande wao kuliko sisi”

“Tulifanikiwa kubadilisha hali ya mchezo kila ilipowezekana. Nakiri kikosi changu kilianza katika morari ya chini. Lakini lengo letu lilikua ni kuwasoma Liverpool kwanza, ili kujua wamejipanga kwa mikakati gani.

Mchezo huo ulikua wa kwanza kwa Jose Mourinho kwenda Anfield akiwana kikosi cha Man Utd tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa meneja wa Mashetani Wekundu akichukua nafasi ya Louis Van Gaal mwishoni mwa msimu uliopita.

Nyasi Bandia Za Nyamagana Zawasili TFF
Neymar Kuandika Rekodi Mpya FC Barcelona