Meneja wa Tottenham Hotspurs Jose Mourinho amekianika hadharani kikosi chake cha kwanza cha muda wote cha mastaa aliowahi kuwanoa, huku akiwaweka pembeni wachezaji wa Manchester United.

Meneja huyo kutoka Ureno “The Special One” aliteuliwa kuinoa Man United Mei 2016, lakini licha ya kushinda taji la Europa League na Kombe la Ligi kwenye msimu wake wa kwanza, hakuwa kabisa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo ya Old Trafford.

Katika kikosi hicho pia hawamo Sergio Ramos, David De Gea, Iker Casillas na Zlatan Ibrahimovic na mshambuliaji wake wa sasa ndani ya Spurs Harry Kane.

Kwenye kikosi hicho, Mourinho amemtaja kipa Petr Cech, aliyekuwa namba moja wake huko Chelsea na mabeki ni John Terry na Ricardo Carvalho, William Gallas na kushoto Javier Zanetti.

Zanetti ni mchezaji pekee kutoka kwenye kikosi cha Inter Milan, ambacho Mourinho alikinoa kati ya 2008 na 2010 na kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwenye safu ya kiungo, Mourinho amemtaka Claude Makelele kiungo mkabaji, huku akishirikiana na Frank Lampard na Mesut Ozil kwenye eneo hilo la katikati ya uwanja.

Ozil alikuwa chini ya Mourinho huko Real Madrid kuanzia 2010 hadi 2013 kabla ya kutua Arsenal.

Kwenye safu ya ushambuliaji, Mourinho amewachagua, Eden Hazard upande wa kulia, Cristiano Ronaldo kulia na mshambuliaji wa kati ni Didier Drogba.

Usajili majira ya kiangazi watajwa England
Jurgen Klopp awabwatukia wachezaji