Imebainika kwamba, mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich, anashindwa kuchukua maamuzi ya kumfuta kazi meneja wa kikosi cha klabu hiyo Jose Mourinho, kutokana na kushindwa kumpata mbadala wake mpaka sasa.

Mwishoni mwa juma lililopita baada ya kikosi cha Chelsea kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Stoke City, taarifa ziliainisha kwamba, Mourinho alikua na matumaini hafifu ya kubaki kibaruani na pengine juma hili angefutwa kazi.

Hali hiyo imekua ngumu kutekelezeka, kutokana na mmiliki wa klabu ya Chelsea kushindwa kufanya maamuzi, kufuatia mameneja anaowakusudia kuchukua nafasi ya Mourinho, kuwa na wakati mgumu wa kukubali ofa ya kuelekea jijini London.

Pep Guardiola pamoja na Diego Simeone wametajwa na mtandao wa Goal.com kuwa katika rada za tajiri huyo kutoka nchini Urusi, lakini mazingira yao ya sasa yanawanyima nafasi ya kukubali kuwa sehemu ya Chelsea.

Hata hivyo haifahamiki ni jambo gani linaloendelea kwa Roman Abramovich, mpaka sasa lakini dalili zinaonyeha huenda Mourinho akabaki kwenye kibarua chache hadi mwishoni mwa msimu huu.

Mara kadhaa meneja huyo kutoka nchini Ureno amekua anazungumzia uwezekano hafifu wa kufutwa kwake kazi klabuni hapo, kutokana na kuamini bado anahitajika kwa udi na uvumba kufuatia falsafa ya ufundishaji wake kuwa na mantiki ya kusaka mafanikio.

Mourinho alirejea Chelsea mwaka 2013, baada ya kumalizana na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, na kwa mara ya kwanza alipita klabuni hapo kati ya mwaka 2004–2007.

Kombe La Dunia 2018, Burundi Yakwama Nyumbani
Jese Rodriguez Amtamanisha Arsene Wenger