Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Olympic Lyon Nabil Fekir huenda akabadili mpango wa kujiunga na majogoo wa jiji Liverpool, na kuelekea kwenye klabu ya Man Utd, ambayo inatajwa kuwa tayari kuingia kwenye vita ya usajili wa mchezaji huyo.

Fekir alikua na matarajio makuibwa ya kutua Anfield yalipo makao makuu ya klabu ya Liverpool kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia huko nchini Urusi, lakini kuvurugika kwa mazungumzo ya uhamisho wake, kulikwamisha mpango huo.

Hata hivyo bado Liverpool wana matumaini makubwa ya kuendelea na harakati za kumsajili kiungo huyo kwa ada ya pauni milioni 62, japo taarifa za Man Utd za kutaka kuingilia kati dili hilo kuwekwa hadharani.

Rais wa klabu ya Olympic Lyon Jean Michael-Aulas amethibitisha kufanya mazungumzo na meneja wa Man Utd Jose Mourinho, ambayo yalilenga usajili wa Fekir, ambaye kwa sasa yupo kwenye majukumu ya kuitumikia timu ya taifa ya Ufaransa kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi.

“Nilikua na Jose Mourinho na tumezungumza baadhi ya mambo kuhusu Nabi Fakir.

“Binafsi niliwahi kufanya mazungumza na Liverpool kuhusu mpango wa usajili wa mchezaji huyu. Lakini bado biashara ipo wazi, wanaweza kuendelea, japo Man Utd nao wameonyesha nia ya kufanya biashara na sisi, baada ya fainali za kombe la dunia.”

Hata hivyo kiongozi huyo amebainisha kuwa, klabu ya Olympic Lyon pia ipo kwenye maandalizi ya kufanya mazungumzo na Fekir kwa ajili ya mkataba mpya, endapo dili la kuondoka kwake litashindwa kukamilika kama walivyokusudia.

” Nimemfahamisha Nabil Fekir kuhusu suala la kusaini mkataba mpya, atakapomaliza majukumu katika upande wa timu ya taifa, tutazungumza na ninaamini muafaka utapatikana, endapo itashindikana kuondoka kwake.

“Yupo tayari kwa mambo yote mawili, lakini hatutofanya haraka ya kuzungumza naye ili tuone ni nani kati ya Liverpool na Man Utd mwenye nia thabit ya kufanya biashara ya kumsajili.

Sokratis Papastathopoulos kutua Arsenal wakati wowote
Argentina waipongeza Croatia kuongoza kundi D

Comments

comments