Aliyekua meneja wa klabu Chelsea, Jose Mourinho amedhamiria kuandika ujumbe kwa mashabiki wa soka duniani kote, ili kuwaaminisha atakuwa mkuu wa benchi la ufundi na Man Utd msimu ujao wa ligi nchini England.

Mourinho amedhamiria kufanya hivyo, kutokana na figusu figisu zinazoendelea kwa sasa, za kutaka kumuondoa kwenye kinyang’anyiro cha kupewa nafasi ya kurithi mikoba ambayo huenda ikaachwa na meneja kutoka nchini Uholanzi, Louis van Gaal.

Aliyekua meneja wa Man Utd kuanzia mwaka 1986-2013, Sir Alex Ferguson, ni mmoja wa wadau wanaopinga zoezi la kuajiriwa kwa Mourinho klabuni hapo, kutokana na kuamini hafai katika falsafa za mashetani wekundu.

Ferguson, alifikia hatua ya kuushauri uongozi wa klabu ya Man Utd, usitishe zoezi la kutaka kumpa ajira meneja huyo kutoka nchini Ureno na kama watashindwa kusaka mtu mwingine badala yake, ni bora waendelee na Van Gaal.

Ushauri huo umeelezwa kuwagawa baadhi ya wajumbe ya bodi ya uongozi wa klabu ya Man Utd, ambao miongoni mwao wanaamini Mourinho sio mtu sahihi na waliosalia wameendelea kusisitiza ni lazima jambo la ajira kwa Mourinho litimizwe mwishoni mwa msimu huu.

Mourinho, anapewa nafasi kubwa ya kukabidhiwa jukumu la kuwa meneja wa Man Utd, kutokana na sifa ya kuwa meneja huru mpaka dakika hii, hivyo haitowagharimu kiasi kikubwa cha fedha viongozi wa klabu hiyo katika mpango wa kumpa ajira, tofauti na mameneja wengine ambao bado wanaendelea na ajira zao.

Hata hivyo haijaelezwa kwa undani kwa nini Mourinho amedhamiria kuandika ujumbe huo kwa wadau wa soka duniani, lakini wadadisi wa masuala ya soka wanaamini anataka kufanya hivyo kama kumjibu Ferguson aliyepinga ujio wake.

Diamond kupiga collabo na Kanye West? Menejimenti zao zawekana sawa
Toni Kroos Anasaka Chaka La Kujifichia Msimu Wa 2016-17