Meneja wa Man Utd Jose Mourinho atajaribu kutuma ofa kwenye klabu ya Borussia Dortmund, ili kufanikisha usajili wa mshambuliaji kinda kutoka Ufaransa Ousmane Dembele.

Jose Mourinho amedhamiria kufanya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, baada ya kuhakikishiwa na wafuatiliaji vipaji wa Man Utd kuhusu uwezo wa Dembele ambaye tayari ameshaifungia Borussia Dortmund mabao sita katika michezo 26 aliyocheza.

Dembele aliwahi kuzikataa klabu za Chelsea, Arsenal na Man Utd zote za England na aliamua kujiunga na Borussia Dortmund akitokea Rennes ya Ufaransa mwaka 2016, kwa kuamini angepata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Endapo mpango wa Jose Mourinho utafanikiwa, utaigharimu Man Utd kiasi cha Pauni milioni 50 ambazo zinatajwa kama thamani halisi ya mshambuliaji huyo.

Hata hivyo Man Utd wameweka mpango mbadala wa usajili, endapo watashindwa kumsajili Dembele mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji anaefikiriwa na klabu hiyo ya Old Traffold kama mbadala wa Dembele, ni mshambuliaji kutoka nchini Croatia na klabu ya Inter Milan ya Italia Ivan Perisic.

Ben Pol kufanya kazi na 'Producer' mkubwa Marekani
Video: Korea Kaskazini yasema iko tayari kwa vita na Marekani