Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho, amesema ni vigumu kwa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Lionel Messi kukubali kuondoka FC Barcelona.

Mourinho amezungumzia suala hilo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari ambao ulihusu mchezo wa Europa League, ambapo Mashetani wekundu watakua nyumbani Old Trafford wakipapatuana na Feyenoord ya Uholanzi.

Waandishi wa habari walimuuliza meneja huyo kutoka nchini Ureno, kama ana mpango wa kuingia katika vita ya kumuwania mshambuliaji huyo ambaye pia anahusishwa na taarifa za kutakiwa na Man City.

Mourinho alisema ni jambo la kushangaza kuona Man utd imeingizwa katika mkumbo wa usajili wa Messi, kutokana na kufahamu kwamba mshambuliaji huyo ni vigumu kuondoka FC Barcelona.

Alisema Messi amejizatiti vilivyo kuendeleza kuchezea ndani ya klabu hiyo ya Cataluña, na wakati mwingine huona wanaodhamiria kumsajili wanapoteza muda.

“Messi amekua na mazingira mazuri FC Barcelona, tena kwa muda mrefu, hivyo ni jambo la kustaajabisha kwa klabu nyingine kujitokeza na kutaka kumng’oa Camp Nou,” Alisema Mourinho

“Kweli kabisa ninawahakikishia, Messi hatoweza kuondoka FC Barcelona na nina matumaini makubwa huenda akamaliza soka lake akiwa kwenye klabu hiyo.

“Kuhusu Man Utd kuhitaji kumsajili, sijui kama linawezekana lakini kwa uhakika ninakwambieni haitowezekana kwa Messi kuondoka FC Barcelona. “Alisisitiza Mourinho.

Silvio Berlusconi Kuiuza AC Milan Disemba 13
Ifahamu Siri Ya Kadi Za Njano Mwishoni Mwa Mwaka