Kocha Jose Pekerman ametangaza kujiuzulu kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Colombia, baada ya miezi miwili iliyoshuhudia akikiongoza kikosi cha cha taifa hilo kwenye fainali za kombe la dunia, na kufika hatua ya 16 bora, kabla ya kuondolewa na England kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Shirikisho la soka nchini Colombia (FCF) limethibitisha kuondoka kwa kocha huyo, ambaye alianza shughuli za kukinoa kikosi cha timu ya taifa mwaka 2012, na kuingoza katika fainali za kombe la dunia mwaka 2014 (Brazil) na 2018 (Urusi).

“Baada ya kikao na Jose Nestor Pekerman, kocha alieleza sababu za kutohitaji nafasi ya kuendelea kukinoa kikosi chetu,” Imeeleza taarifa iliyotolewa na FCF.

“Sisi kama FCF tunajivunia kufanya kazi na kocha huyu ambaye ni raia wa Argentina, na tunamshukuru kwa msaada wake mkubwa ambao ulituwezesha kushiriki fainali za kombe la dunia za 2014 na 2018.”

“Ametuambia anahitaji kubadilisha mazingira ya kazi yake, tulimbembeleza aendelee kufanya kazi na sisi, lakini aliendelea kuhitaji nafasi ya kuondoka hapa Colombia, tumeheshimu maamuzi yake na tunamtakia kila la kheri huko aendapo.”

Taarifa za awali zinadai kuwa Pekerman anatajwa kuwa mmoja wa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kutangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la  kikosi cha Mexico ama Argentina.

Pekerman aliwahi kukiongoza kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 cha Argentina, na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia mara tatu (1995, 1997 na 2001).

Shirikisho la soka nchini Colombia tayari limeshamtangaza Arturo Reyes kuwa kocha mkuu wa muda, na atakiongoza kikosi cha nchi hiyo katika mpambano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Venezuela utakaochezwa mjini Miami-Marekani Septemba 07 na siku nne baadae dhidi ya Argentina mjini New Jersey-Marekani.

Akutwa na Vijiko, Viberiti, Mswaki, tumboni
Marekani yatafakari kuwaondoa Makomando wake Afrika